Wakati wa kupatiwa chanjo yako

Maelezo au taarifa zifuatazo zimetengenezwa kwa ajili ya tovuti hii na wataalamu wa tiba na afya ya jamii kwa kutumia vyanzo au taarifa kutoka katika serikali ya Canada na vingine vya kisayansi na tiba. Hayajakusudiwa kuwa ushauri wa kitabibu. Mara zote unashauriwa kupata ushauri kutoka kwa watoaji huduma ya afya waliofuzu ukiwa na maswali yoyote kuhusu chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19).

Kumbukumbu au rekodi ya chanjo yako itahifadhiwa na mamlaka ya afya ya jimbo au wilaya/mkoa wako. Kwa ujumla, utapewa nakala yako ya karatasi au kielektroniki. Tafadhali cheki na mamlaka ya afya ya eneo lako au kliniki utakapopatia chanjo kuelewa kwamba utapewa nyaraka zipi.

Ndio, unaweza kuja na mtu ili akusaidie kwenye mchakato wa kupatiwa chanjo, au kama unahitaji msaada au huduma ya ukalimani, unaweza kuja na mtu.

Unatakiwa kuleta nakala ya kuchapishwa au kielektroniki kuthibitisha miadi yako (usajili). Unatakiwa pia kuja na kadi yako ya afya kama unayo.