REWARDS FOR CHANGE

Join This Is Our Shot in getting Canada #TogetherAgain. Enter for a chance to win one of thousands of prizes across Canada in Rewards for Change.

This Is Our Shot kuwa
#TogetherAgain

Play Video

Unatamani kufanya mambo gani ambayo umeshindwa kutokana na gonjwa hili-kufurahi au kujumuika na familia na marafiki, kuhudhuria mechi za michezo au kwa kifupi kujumuika? Sote tunataka mambo haya yarudi.

This Is Our Shot kuwa #TogetherAgain ni harakati inayolenga kuwaunganisha watu wote waishio nchini Canada na kuwahamasisha kutokusita kupatiwa chanjo na badala yake kuwa na imani au ujasiri ili tuteketeze gonjwa hili-kwa pamoja.

Ili kuwa #TogetherAgain, lazima tuendelee kujikinga sisi wenyewe, familia zetu, na jamii zetu. Tuanze kwa kutambua kwamba kupatiwa chanjo sio rahisi kwa baadhi ya watu kama ilivyo kwa wengine. Lazima sote kwa pamoja tuhakikishe kwamba kila mtu ana uwezo wa kupata taarifa sahihi na maelezo wanayohitaji ili kufanya au kuchukua maamuzi sahihi.

This Is Our Shot kuteketeza au kumaliza gonjwa hili nchini Canada

MAELEZO KUHUSU CHANJO YA COVID-19(UVIKO-19)

[XXXXX] ya chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) zimeshatolewa kwa watu nchini Canada

Unaweza kuwa na maswali kuhusu chanjo. Tupo hapa kukusaidia kwa kukupa taarifa/maarifa unayohitaji ili ujisikie kuwa na imani au ujasiri wa kupatiwa chanjo na hivyo kusaidia kuteketeza gonjwa hili.

Pata taarifa sahihi. Hii ndio nafasi yetu ya kipekee ili kuweza kujumuika pamoja tena.

Utakapokuwa tayari kuweka miadi…

Bonyeza kwenye jimbo lako na kisha utapelekwa kwenye sehemu ya jimbo lako ya kuwekea miadi. Au nenda/tembelea Vaccine Hunters Canada ambao utakusaidia kukuongoza kwenda kwenye kliniki cha chanjo nchi nzima, yakiwemo maduka ya dawa.

57,020

[XXXXX] ya chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) zimeshasambazwa

52,913

[XXXXX]ya chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) zimeshatolewa kwa watu nchini Canada

Data kutoka kwa Serikali ya Canada
https://art-bd.shinyapps.io/covid19canada/

Mikutano ya Hadhara ya Moja kwa Moja

This Is Our Shot kuwa #TogetherAgain mikutano ya mara kwa mara ya hadhara kuhusu taarifa au maelezo ya COVID-19 (UVIKO-19).

Unawezakutuma maswali yako kabla au wakati wa mkutano.

Tukio litakuwa kwa lugha ya Kiingereza.

INAPATIKANA KATIKA LUGHA MBALIMBALI

Jinsi ya kushiriki

Kampeni ya This Is Our Shot kuwa #TogetherAgain

Yeyote anaweza kushiriki na kwa kufanya hivyo, utasaidia kusambaza ujumbe kwamba chanjo inaweza kumaliza gonjwa hili nchini Canada.

  1. Pata chanjo zamu yako itakapofika.
  2. Shiriki kwenye kampeni ya #ThisIsOurShotCA #TogetherAgain kwa kununua shati/tisheti .
  3. Vaa shati/tisheti yako utakapokwenda kwenye miadi ya chanjo na kutunuku bandeji ya chanjo yako kwa mtu (au kitu) unayemjali.
  4. Weka picha au video ukiwa umevaa shati/tisheti yako inayoonyesha bandeji yako, kisha tagi marafiki zako na familia na kuwaomba na wao wafanye hivyo hivyo.
  5. Pia weka picha,video au machapisho yako kwa kutumia #ThisIsOurShotCA #TogetherAgain kusaidia kusambaza ujumbe.

Mapato yote yatakwenda kwa shirika la hisani la Kids Help Phone.

Kuhusu This Is Our Shot kuwa #TogetherAgain

Mashirika ya msingi/kijamii, wafanyakazi wa masuala ya afya kote nchini Canada na baadhi ya mashirika yanayojulikana sana yaliona haja ya kusambaza ujumbe kuhusu usalama wa chanjo na kuondoa hali ya kusita na badala yake kuwapa watu ujasiri au imani. Yamedhamiria kufanya kazi kwa pamoja kama kundi la umoja, kwa kuzingatia jitihada ya pamoja ambayo itakuwa madhubuti ili kuondokana na hali ya watu kusita kupatiwa chanjo.

Sasa chini ya bango moja la This Is Our Shot kuwa #TogetherAgain wafanyakazi wa masuala ya afya, wafanyakazi wa mstari wa mbele, jamii za maeneo tunayoishi, mashirika na makampuni nchini Canada, na mtandao wa watu mashuhuri, wanajitolea muda na rasilimali zao kukuza ujasiri au imani ya chanjo kwa watu waishio nchini Canada.

Habari za Hivi Karibuni

Watch the full interview: https://www.cp24.com/video?clipId=2221114

Hospital News: Co-led by Dr. Anju Anand, a respirologist at…

Read more

Breakfast Television: Dina and Sid chat with Olympian Clara Hughes…

Read more