Kuhusu chanjo za COVID-19 (UVIKO-19)

Maelezo au taarifa zifuatazo zimetengenezwa kwa ajili ya tovuti hii na wataalamu wa tiba na afya ya jamii kwa kutumia vyanzo au taarifa kutoka katika serikali ya Canada na vingine vya kisayansi na tiba. Hayajakusudiwa kuwa ushauri wa kitabibu. Mara zote unashauriwa kupata ushauri kutoka kwa watoaji huduma ya afya waliofuzu ukiwa na maswali yoyote kuhusu chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19).

Chanjo dhidi ya COVID-19 (UVIKO-19) itasaidia kukulinda usiugue au kufariki kutokana na COVID-19 (UVIKO-19). Pia, itasaidia kukomesha kusambaa kwa COVID-19 (UVIKO-19) nchini Canada, idadi ya kutosha ya raia au watu waishio nchini Canada wanahitaji kupatiwa chanjo kukomesha maambukizi ya kirusi kwenye jamii.

Hata kama mtu hatofariki kutokana na COVID-19 (UVIKO-19), wanaweza kuwa na matatizo ya muda mrefu ya kiafya ikiwemo kupoteza kumbukumbu, matatizo ya kupumua yasiyoelezeka, na madhara au uharibifu kwenye mapafu na moyo.

Ikiwa idadi ya kutosha ya watu watakuwa na kinga, bila shaka kirusi hakitoweza kusambaa. Tunahitaji kupata chanjo angalau asilimia 75% ya idadi ya watu ili kufikia kinga ya kundi/sehemu kubwa ya jamii na hivyo kuendelea na maisha yetu ya kila siku kama hapo awali, kufungua biashara, kukumbatiana na kuwaona tena wapendwa wetu.

Hapana, chanjo zote za COVID-19 (UVIKO-19) hutolewa bure.

Katikati ya mwezi wa Juni, Kamati ya Kitaifa kuhusu Ushauri wa Chanjo (NACI) ilirekebisha mapendekezo yake kuhusiana na kuchanganya chanjo za COVID-19 za dozi ya pili. Chanjo ya mRNA sasa inapendekezwa kama dozi ya pili kwa watu ambao walipokea dozi ya kwanza ya AstraZeneca, kulingana na ushahidi unaoibuka wa uwezekano wa kuwa na kinga bora kutokana na kuchanganya chanjo hizo.

Ikiwa ulipokea chanjo ya mRNA (Pfizer-BioNTech au Moderna) kama dozi yako ya kwanza, utapewa chanjo ya mRNA kama dozi yako ya pili. Inapendekezwa kuwa upokee chanjo ya aina ileile kama uliyopewa mara ya kwanza, isipokuwa iwe haipatikani kwa urahisi au haijulikani, katika hali hiyo ni sawa kupokea aina nyingine ya chanjo ya mRNA. Zote mbili ni salama na zinafanya kazi vizuri.

Ikiwa ulipokea AstraZeneca kama dozi yako ya kwanza, unaweza kuchagua kupata AstraZeneca kama dozi yako ya pili, lakini NACI sasa inapendekeza uchukue chanjo ya mRNA kama dozi yako ya pili.

Chanjo zote zilizoidhinishwa kutumiwa nchini Canada kwa usawa na kwa ufanisi hupunguza kulazwa hospitalini na ugonjwa mbaya, na zote zina ufanisi wa karibu 100% katika kuzuia kifo kinachotokana na COVID-19.

Jambo muhimu ni kwamba hupaswi kusubiri kupata chanjo ya dozi mbili kwa ulinzi kamili. Aina mpya za virusi zinaibuka ambazo zinasababisha visa vingi, kulazwa hospitalini na vifo, na watu wengi kupata chanjo ndio njia pekee ya kukomesha visa hivi.

Kwa mujibu wa Health Canada, na kutokana na majaribio ya kitabibu yaliyohusisha maelfu ya wapokeaji wa chanjo:

Pfizer-BioNTech ni madhubuti kwa asilimia 95% baada ya dozi mbili.

Chanzo: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/pfizer-biontech.html

Moderna ni madhubuti kwa asilimia 94% baada ya dozi mbili

Chanzo: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/moderna.html

AstraZeneca ni madhubuti kwa asilimia 62% baada ya dozi mbili (asilimia 79% kwenye tafiti za Amerika ya Kaskazini/Kusini)
Data halisi kutoka duniani kote zinaonyesha kwamba AZ ni madhubuti kwa asilimia 80%-90% kuzuia watu kulazwa hospitalini.

Chanzo: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/astrazeneca.html

Johnson & Johnson ni madhubuti kwa asilimia 66% baada ya dozi moja na data halisi kwendana na wakati zinaonyesha ni madhubuti kwa asilimia >90% katika kuzuia ukali wa maradhi au ugonjwa na kulazwa hospitali.

Chanzo: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/janssen.html

Chanjo zote nne ni madhubuti kwa kiwango cha juu kwenye kuzuia makali ya COVID-19 (UVIKO-19), kulazwa hospitalini na kifo.

Hiyo inatofautiana kati ya chanjo na aina tofauti/mpya ya virusi.

Kila chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19) itazuia makali ya ugonjwa/kifo kutokana na aina tofauti/mpya za virusi zilizopo nchini Canada hivi sasa.

Hata chanjo zinapoonyesha umadhubuti wa kiwango cha chini dhidi ya aina tofauti za virusi, watengenezaji wa chanjo wanatengeneza au kuunda matoleo mapya ya chanjo zao kuwa bora zaidi dhidi ya aina tofauti/mpya za virusi, ili pengine upate dozi za nyongeza au kuongeza nguvu katika siku za mbeleni ambazo zitakuwa madhubuti kwa miezi na miaka ijayo.

Kwa Pfizer-BioNTech, Moderna na AstraZeneca dozi mbili zinahitajika kwa sababu dozi ya kwanza “inauandaa” mwitikio wa kinga wa mwili wako: mwili wako unajifunza kutengeneza kingamwili za kupambana na COVID-19 (UVIKO-19). Dozi ya pili “inauongezea” kuwa na kinga yenye nguvu zaidi na inayodumu kwa muda mrefu zaidi. Dozi zote zinahitaji ili kutoa kinga kamili.

Chanjo ya Johnson & Johnson imefanyiwa majaribio na kuonekana kuwalinda watu na kutoa kinga kwa dozi moja.

Pfizer-BioNTech na Moderna: chanjo za mRNA.

Kipande kidogo cha mRNA kinachofanya COVID-19 (UVIKO-19) kuongeza protini kinaingia kwenye seli na kuufundisha mwili wako kutengeneza kingamwili dhidi ya virusi vya COVID-19 (UVIKO-19). Kisha mRNA huharibiwa ndani ya masaa machache, na kuacha nyuma mafundisho au maelekezo.

Astra Zeneca na J&J: chanjo za virusi vya vekta.

Chanjo hizi zinatumia kirusi ambacho hakina madhara (kama cha homa ya mafua ya kawaida) ambacho kimepunguzwa nguvu na kisha kurekebishwa kwa kuongezewa kipande cha kirusi cha COVID-19 (UVIKO-19) kuongeza protini ya kirusi. Mchakato huo huo unatokea kama ilivyo kwa chanjo za mRNA hapo juu, kusababisha mwili wetu utengeneze kingamwili na kuamsha seli zetu zingine za kinga.

Miongoni mwa chanjo zote hizo hakuna inayoingiliana au kubadilisha vinasaba (DNA)

Hakuna yenye virusi hai vya COVID-19 (UVIKO-19).

Zote zina madhara mengine ya kiafya yanayofanana: maumivu kwenye sehemu ulipochomwa, uchovu, homa au dalili kama za mafua, maumivu ya kichwa, maumivu kidogo ya misuli/viungo.

Health Canada imeidhinisha matumizi ya chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) Pfizer-BioNTech, Moderna, AstraZeneca na Janssen (Johnson & Johnson) nchini Canada.

Hapana. Kupata chanjo yoyote, ikiwemo ya COVID-19 (UVIKO-19), hakutoathiri majibu ya vipimo vya COVID-19 (UVIKO-19) kwa sababu sio chanjo hai au inayoishi.