Baada ya chanjo yako

Maelezo au taarifa zifuatazo zimetengenezwa kwa ajili ya tovuti hii na wataalamu wa tiba na afya ya jamii kwa kutumia vyanzo au taarifa kutoka katika serikali ya Canada na vingine vya kisayansi na tiba. Hayajakusudiwa kuwa ushauri wa kitabibu. Mara zote unashauriwa kupata ushauri kutoka kwa watoaji huduma ya afya waliofuzu ukiwa na maswali yoyote kuhusu chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19).

Hatuwezi kusema kwa uhakika, lakini inawezekana ukaendelea kuwa au kupatwa na kirusi hata kama umepata chanjo. Tunajua kwamba chanjo itakukinga usiugue kutokana na kirusi, lakini inawezekana ukaendelea kuwa au kupatwa na kirusi na unaweza kuambukiza wengine ingawa umepata chanjo. Tutajifunza zaidi kadri majaribio ya kitabibu yanavyoendelea na ushahidi wa uhakika kutoka duniani kote unavyojitokeza. Kwa wakati huu, tunahitaji kuendelea kuvaa barakoa zetu, kutokaribiana sana na watu na kuendelea kufuata ushauri wa watu wa afya jamii mpaka hapo wa-Kanada wa kutosha watakapopatiwa chanjo kamili.

Inachukua takribani wiki mbili baada ya dozi ya pili kwa mwili kujenga kinga baada ya kupatiwa chanjo. Mtu anaweza kuambukizwa kirusi kabla au baada tu ya kupatiwa chanjo na kuugua kwa sababu chanjo haikupata muda wa kutosha kutoa ulinzi/kinga.

Hii ndio pia kwanini mfululizo kamili wa dozi mbili za chanjo unahitajika.

Uthabiti wa awali wa chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19) tayari ni wa hali ya juu sana baada ya dozi ya kwanza (80-92%) na unadumu au kubakia hivyo kwa angalau miezi michache.

Uzoefu na chanjo zingine za dozi anuwai baada ya dozi moja zinaonyesha kinga inayoendelea inaweza kudumu kwa miezi sita au zaidi. Kwa kweli, tafiti nyingi zimeonyesha kuwa unapata kinga bora zaidi ya kukabiliana na ugonjwa unaposubiri kwa muda mrefu. Kwa hivyo jambo hilo linaungwa mkono na sayansi.

Na kwa chanjo nyingi, viwango vya kingamwili (kinga ya mwili) vitashuka baada ya muda fulani na sio kuanguka ghafla chini ya viwango vya kutoa kinga. Hata miezi au miaka baadaye, dozi nyingine ya chanjo inaweza kuongeza kinga mwilini kwa viwango vya juu, ikitoa kinga ya muda mrefu.

Kwa kuwa sasa tuna chanjo ya kuaminika zaidi nchini Canada, ratiba kati ya dozi moja na nyingine imepunguzwa hadi wiki nane.

Ndiyo, kwa sasa, hadi Wakala wa Afya ya Umma wa Canada watakapoamua ni wakati gani mzuri wa kuacha kuvaa maski na wa kuacha kuweka umbali kati ya mtu mmoja na mwingine. Hii ni kwa sababu inachukua wiki kadhaa kwa chanjo hiyo kuwa na ufanisi (kujenga kinga mwilini) na ulinzi wa kiwango cha juu unapatikana tu baada ya kukamilika kwa dozi ya pili ya chanjo za COVID-19 za Pfizer-BioNTech, Moderna na AstraZeneca, kwa watu wengi iwezekanavyo.

Bado hatujui kinga/ulinzi unadumu kwa muda gani kwa waliopatiwa chanjo. Tafiti juu ya chanjo za mRNA kwa sasa zinaonyesha kwamba watu waliopatiwa chanjo wana kinga yenye nguvu sana dhidi ya COVID-19 (UVIKO-19) kwa angalau miezi sita. Inaonekana kinga itadumu kwa muda, lakini tafiti zinahitaji kufuatilia hili baada ya muda.

Kwa wakati huu, hatuna uhakika kama kinga itadumu kwa mwaka mmoja au miaka kumi, au kama patakuwa na haja ya chanjo ya kuiongezea nguvu baada ya muda fulani.

Kwa kawaida inachukua wiki kadhaa kwa mwili kujenga kinga baada ya kupatiwa chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19). Lakini kumbuka kwamba dozi mbili zinahitajika ili kupata kinga bora kutoka kwenye chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) kutoka Pfizer-BioNTech, Moderna na AstraZeneca. Chanjo ya Johnson & Johnson inahitaji dozi moja tu.

Baada ya chanjo, ni kawaida kuwa na madhara mengine kidogo ya afya na ya muda mfupi ikiwemo:

  • Maumivu, wekundu, hali ya joto, kuwashwa na kuvimba sehemu iliyochomwa,
  • Uchovu,
  • Maumivu ya kichwa,
  • Kichefuchefu,
  • Maumivu ya misuli au viungo vya mwili na
  • Homa kidogo au kutetemeka.

Hizi ni dalili za kawaida kwamba mwili wako unajenga kinga/ulinzi na dalili hizi zitatoweka baada ya siku chache.

Kama dalili ni kubwa au zinaongezeka, onana na mtoaji huduma ya afya. Kama dalili zinafanana na za COVID-19 (VIUKO-19),unapaswa kupimwa na kujitenga mpaka pale majibu yatakapopatikana.

Kwa nadra sana, madhara mengine ya kiafya ya chanjo yanayoitwa anafilaksisi yanaweza kujitokeza. Kwa ujumla hii hutokea ndani ya dakika chache au saa moja baada ya chanjo. Kwa sababu hii, watu wanaopatiwa chanjo ya COVID-19 (VIUKO-19) hutakiwa kubakia sehemu walipopatiwa chanjo kwa angalau dakika 15 baada ya chanjo ili watumishi wa huduma ya afya waweze kufuatilia au kumsimamia aliyepatiwa chanjo kuona kama kuna athari (reactions) mbaya/mzito.

Madhara mengine ya kiafya sio kiashirio kwamba chanjo inafanya kazi au la.

Ni kweli kwamba madhara mengine ya kiafya ni dalili za kawaida kwamba chanjo inafanya kazi na mwili wako unajenga kinga/ulinzi. Hata hivyo, hii haimaanishi uwe na wasiwasi au mashaka kama huoni madhara yoyote. wa mfano, chanjo za mRNA zilitoa kinga kwa zaidi ya asilimia 90% ya waliopatiwa kwenye majaribio ya kitabibu, lakini zaidi ya asilimia 50% hawakupata madhara yoyote. Kwa maneno mengine, watu hawakupata athari lakini walipata kinga kamili.

Kwa hiyo endapo huoni madhara yoyote ya kiafya baada ya chanjo yako ya COVID-19 (UVIKO-19), sio jambo la kukutia wasiwasi au mashaka-bado una kinga sawa na mtu ambaye hakuona au kuhisi madhara ya pembeni.