Afya na usalama wa chanjo

Maelezo au taarifa zifuatazo zimetengenezwa kwa ajili ya tovuti hii na wataalamu wa tiba na afya ya jamii kwa kutumia vyanzo au taarifa kutoka katika serikali ya Canada na vingine vya kisayansi na tiba. Hayajakusudiwa kuwa ushauri wa kitabibu. Mara zote unashauriwa kupata ushauri kutoka kwa watoaji huduma ya afya waliofuzu ukiwa na maswali yoyote kuhusu chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19).

Endapo unajiuliza kama unastahiki kupata chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19) kwenye mkoa au eneo lako, au unataka kuweka miadi ya kupata chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19), bonyeza kwenye kiungo kilichopo hapo chini kuona taarifa za wakati huu na fursa au chaguzi za miadi za mahali unapoishi.

British Columbia
Alberta
Saskatchewan
Manitoba
Ontario
Quebec
New Brunswick
Nova Scotia
Newfoundland and Labrador
Prince Edward Island
Northwest Territories
Nunavut
Yukon

Chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) zilizoidhinishwa kwa matumizi nchini Canada hazijatengenezwa au kuwa na mchanganyiko wa mayai, jelatini (gundi-gundi), nyama ya nguruwe, nyama ya ng’ombe, masalia ya kijusi(fetal),zebaki, thimerosali, au mpira na hazina kiambato(ingredient) ambayo imewekewa vikwazo kwa sababu za lishe au dini.
Orodha kamili ya vitu au mchanganyiko uliotumika kutengeneza kila chanjo unaweza kupatikana katika:

Pfizer-BioNTech: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/pfizer-biontech.html

Moderna: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/moderna.html

AstraZeneca: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/astrazeneca.html

Johnson & Johnson: https://www.canada.ca/en/health-canada/services/drugs-health-products/covid19-industry/drugs-vaccines-treatments/vaccines/janssen.html

Hakuna hatua iliyorukwa au kuvukwa, na taratibu zote za kiusalama zilifuatwa. Chanjo zilitengenezwa haraka kutokana na maendeleo ya kiteknolojia na kwa sababu ruhusa za sehemu au masuala yasiyo ya kitabibu (urasimu wa mchakato na ruhusa au mihuri) zilipelekwa upesi.

Hapana. Protini iliyotumika kamwe haiingiliani na au kubadili vinasaba vyako (DNA). Huharibiwa kiasili au kawaida ndani ya masaa machache, na kuacha mafundisho au maelekezo ya jinsi ya kutengeneza kingamwili endapo utapatwa au kuambukizwa virusi vya COVID-19 (UVIKO-19).

Chanjo ya Pfizer-BioNTech imeidhinishwa na kuthibitishwa na Health Canada kwa watoto walio na umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea.

Chanjo za Moderna, AstraZeneca na Johnson & Johnson zimeidhinishwa na kuthibitishwa na Health Canada kwa matumizi ya watu wazima kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Hivi sasa tafiti zinafanyika kubainisha usalama na umadhubuti au ufanisi wa chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) kwa watoto wadogo.

Hivi sasa nchini Canada, chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) hazipaswi kutolewa wakati mmoja na chanjo zingine. Hata hivyo, nchini Marekani, chanjo za COVID-19 (UVIKO-19) zinaweza kutolewa pamoja na chanjo zingine bila kujali muda, ikiwemo kutolewa kwa chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19) na chanjo zingine siku hiyo hiyo. Unatakiwa kujadiliana na mtoaji wako wa huduma ya afya kama hii imeashiriwa kwako.

Karibuni kila mtu ataweza kupatiwa chanjo kwa usalama au bila matatizo yoyote, ingawa idadi ndogo sana ya watu watatakiwa kuepuka chanjo kutokana na mzio (allergy) mkali unaoweza kutokana na baadhi ya vitu vilivyotumika kutengeneza chanjo. Kwa muktadha wa hatari zinazoendelea za COVID-19 (UVIKO-19), watu wengi wanaweza kupatiwa chanjo. Kimsingi, watu walio na maradhi mengine tayari wanaweza kuwa kwenye hatari zaidi kutokana na matatizo yatokanayo na maambukizi ya COVID-19 (UVIKO-19) na hivyo wanatakiwa kupata chanjo mapema iwezekanavyo kutokana na upatikanaji wake.

Kwa ujumla, ni salama kupata chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19) hata kama upo mbioni kupona kutoka kwenye maradhi (mfano,.vipele au mkanda wa jeshi), lakini kama una ugonjwa mpya unaokuzuia kufanya kazi zako za kawaida, unapaswa kusubiri kupatiwa chanjo mpaka utakapopona. Hii itakusaidia kutofautisha madhara mengine ya kiafya yanayoweza kujitokeza kutokana na chanjo na hali ya ugonjwa wako kuwa mbaya zaidi. Pia, kusubiri mpaka utakapopona kutahakikisha kwamba huhatarishi maisha ya wengine kwa kuwaambukiza utakapokuja kupata chanjo.

Kama una dalili za COVID-19 (UVIKO-19),unatakiwa kukaa nyumbani na kufanyiwa vipimo.

Karibuni kila mtu anaweza kupatiwa chanjo kwa usalama au bila matatizo yoyote. Hakuna wasiwasi au mashaka kuhusu usalama kwa wale wenye kinga ya mwili iliyopungua nguvu au ugonjwa wa kingamwili. Inawezekana chanjo isifanye kazi kama ilivyotarajiwa kwa watu ambao wana mfumo wa kinga ya mwili uliopungua nguvu. Kama una maswali na una mfumo wa kinga ya mwili uliopungua nguvu au ugonjwa wa kingamwili, ongea na mtoaji huduma ya afya Kuhusu chanjo za COVID-19 (UVIKO-19).

Mzunguko wa hedhi ni mchakato mgumu au tata, na unaweza kuathiriwa na mambo mengi kama vile, mabadiliko ya kimazingira, msongo wa mawazo, ulalaji na baadhi ya dawa. Ukuta wa mfuko wa uzazi kimsingi unachukuliwa kuwa sehemu hai ya mfumo wa kinga wa mwili. Mfumo wako wa kinga unapofanya kazi ya ziada kwa sababu umepatiwa chanjo au unaumwa, unaweza pia kuona mabadiliko ya jinsi endometriamu inavyoitikia. Kwa njia hii inawezekana chanjo ikaathiri kwa njia moja au nyingine mzunguko wako wa hedhi.

Lakini, jambo moja la kuzingatia ni kwamba wakati wowote unapotizama kundi kubwa la watu, mara zote kutakuwa na watu wanaopatwa na mabadiliko kwenye mzunguko wao wa hedhi. Katika mamilioni ya watu wanaopatiwa chanjo duniani kote, kutakuwa pia na watu wanaopatwa au kuwa na mabadiliko kwenye mizunguko yao ya hedhi. Watafiti wanaamini kwamba chanjo ni salama, na kwamba hakuna data au taarifa za kutosha kuonyesha au kupendekeza kwamba kunatakiwa kuwa na wasiwasi au mashaka kutokana na mabadiliko kwenye mzunguko wa hedhi unaoweza kujitokeza.

Chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19) haitolewi baada ya chanjo, kwa hiyo kuzungukwa na watu ambao wamepatiwa chanjo hivi karibuni hakutarajiwi kuathiri mzunguko wa hedhi wa mtu mwingine.

Mabadiliko yoyote unayoweza kuyapata au kuyapitia kwenye mzunguko wako wa hedhi baada ya kupata chanjo ni ya muda mfupi, kwa hiyo isiwe sababu ya wewe kutopata chanjo. Hata hivyo, wanawake walio na wasiwasi au mashaka wanapaswa kuongea na daktari kwa sababu mzunguko wa hedhi unaweza pia kucheleweshwa na sababu zingine.

Canadian Society of Obstetrics and Gynecology (SOGC), Kamati ya Kitaifa ya Ushauri Kuhusu Chanjo na wataalamu wa afya jamii nchini Canada wote wanashauri kwamba wanawake wajawazito au wanaonyonyesha wapewe kipaumbele na kupewa chanjo wakati wowote (kila miezi mitatu ya ujauzito) wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha endapo wana haki au wakati wao wa kupata chanjo umefika na kama hakuna hali inayopingana. Kama una maswali, na ni mjamzito, unapanga kupata ujauzito au unanyonyesha, ongea na mtoaji huduma ya afya kuhusu chanjo za COVID-19 (UVIKO-19).

Hakuna ushahidi kwamba chanjo yoyote, ikiwemo ya COVID-19 (UVIKO-19), inaathiri uwezo wa kuzaa/kuzalisha aidha kwa wanawake au wanaume.

Kuna sababu chache sana kwa mtu kutopata chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19).

Usipate chanjo kama una:

1.Mzio (allergy) mkali dhidi ya vitu vyoyote vilivyotumika kutengeneza chanjo: mchanganyiko wa chanjo za mRNA ambao umehusishwa na mzio mkali lakini wa nadra (anafilaksisi) ni polyethilini glycoli (PEG), ambayo inaweza kupatikana kwenye vipodozi, bidhaa za kutunza ngozi ya mwili, vilainisha choo, baadhi ya vyakula vya kusindikwa, vinywaji na bidhaa zingine. Zingatia: PEG haipo kwenye chanjo za AstraZeneca na Johnson & Johnson. Kiambato (ingredient) kilichomo kwenye chanjo za AstraZeneca na Johnson & Johnson ambacho kimehusishwa na mzio (allergy) mkali lakini wa nadra ni Polysorbate 80—Kinapatikana pia kwenye maandalizi ya kitabibu (kwa mfano mafuta ya vitamini, tembe na ajenti za kuua kansa) na vipodozi.

2.Umewahi kuwa na athari (reaction) ya kuhatarisha maisha kwenye dozi yako iliyopita ya COVID-19 (UVIKO-19) au kwa kiambato chochote cha chanjo.

Ongea na mtoaji wako wa huduma ya afya kama umewahi kupatwa na athari (reaction) wa anafilaksisi lakini hujui kilichosababisha. Mzio (allergy) mkali unaotishia maisha kutokana na chanjo (anafilaksisi) hutokea kwa nadra sana kuliko watu wanavyofikiri. Anafilaksisi mara nyingi inazuilika na inatibika kwa vyovyote vile. Watoaji wote wa huduma ya kiafya ya chanjo nchini Canada wanatakiwa kuwa wamefundishwa na hutizama kwa makini wakati wa utoaji wa chanjo na kuwa tayari kutibu anafilaksisi mara moja. Mara chache sana, kutegemea na ushauri au mapendekezo ya mtaalamu wa mzio au Ofisa wa Matibabu ya Afya, mtu anaweza kupatiwa chanjo katika mazingira ya hospitali.

Haishauriwi kunywa pombe au kuja kwenye miadi yako ya chanjo ukiwa umelewa. Hii sio kwa sababu ya wasiwasi au mashaka juu ya usalama wa chanjo (kwamba labda pombe inaweza kuingiliana na chanjo) bali kwa sababu mtoaji wako wa huduma ya afya anahitaji ridhaa yako kabla ya kukupatia chanjo. Pombe inaweza kuharibu (kupunguza) uwezo wako wa kuelewa kikamilifu taarifa au maelezo ya afya yanayotolewa na kuuliza maswali.

Hakuna tafiti kuhusiana na matumizi ya pombe na umadhubuti wa chanjo za COVID-19 (UVIKO-19). Watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa matumizi ya pombe (AUD) wanaweza kuwa na mfumo wa kinga yenye hilitafu (dhaifu) na wanapaswa kuongea na watoaji wao wa huduma ya afya. Maoni ya wataalam ni kwamba hatutarajii kiwango kidogo cha matumizi ya pombe kuwa na athari hasi kwenye mwitikio wa kinga kwa chanjo.

Kama unatumia bangi, chanjo ya COVID-19(UVIKO-19) ni salama kwako.

Ila wakati wa miadi yako, tunashauri usiwe umevuta. Hii sio kwa sababu ya wasiwasi au mashaka juu ya usalama wa chanjo (kwamba labda bangi inaweza kuingiliana na chanjo) bali kwa sababu mtoaji wako wa huduma ya afya anahitaji ridhaa yako kabla ya kukupatia chanjo. Bangi inaweza kuharibu (kupunguza) uwezo wako wa kuelewa kikamilifu taarifa au maelezo ya afya yanayotolewa na kuuliza maswali.

Hakuna tafiti kuhusu matumizi ya bangi na umadhubuti wa chanjo za COVID-19 (UVIKO-19). Kuna ushahidi unaochipukia unaoonyesha kwamba uvutaji bangi unaweza kuwa na matokeo hasi kwenye mfumo wa upumuaji wa mtu na ustadi wa kinga kwa hiyo ni muhimu sana kupata chanjo ya COVID-19 (UVIKO-19) kujilinda dhidi ya virusi ikiwa unavuta.